
Mtayarishaji wa filamu na mwigizaji pia William J. Mtitu amesema kuwa maneno aliyoyasema Rais Dr. Jakaya M. Kikwete ndiyo imekuwa chachu ya yeye kufungua kampuni na kusambaza kazi zake na kuachana na kampuni aliyokuwa akifanya nayo kazi awali, tukio hilo lilitokea wakati wa kifo cha marehemu Kanumba.
“Kwanza nikiri kuwa maneno ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhesimiwa Dr. Jakaya Kikwete aliyotamka siku aliyoiita Ikulu kamati ya mazishi ya marehemu Steven Kanumba ndiyo yamekuwa yakinisukuma sana hadi kufikia uamuzi huu mzito, sisi pamoja na umaarufu wetu hatuna kitu,”anasema Mtitu.
Mtitu kupitia kampuni yake ya 5 Effects Movie Ltd amefanikiwa kusambaza filamu yake ya Omega Confusion na kuona faida jambo ambalo anapenda kuwashauri wasanii wenzake wenye majina kufanya maamuzi magumu ili kulinda haki zao, siyo kuuza na kubaki na majina tu bila kumiliki kazi zao.
Mtitu ndiyo aliyeibua vipaji vya wasanii kama Aunt Ezekil, Yusuf Mlela, Mariam Ismail na wasanii wengi nyota baada ya mafanikio ya kazi hiyo anatarajia kutoa filamu yake ya Nyati katika kuwadhitishia wasanii wenzake kuwa hata bila wasambazaji wakubwa inawezekana.