PROFESSA JAY AFUNGUA 'MWANALIZOMBE STUDIO'
BAADA ya kufungua saloon ya kiume na kuona inamlipa msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini miondoko ya Hip Hop Joseph Haule 'Professa Jay' sasa afungua rasmia studio ya kurekodi muziki.
Studio hiyo aliyoipa jina la Mwanalizombe ipo maeneo ya Msasani jijini Dar es Salaam, ambayo teyari
imeshakamilika kwa kuwa na vifaa vyote vya kutendea kazi ambapo producer wa studio hiyo anajulikana kwa jina la Duke Touchez.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii Professa Jay aliweka wazi kuwa dhumuni la kufungua studio hiyo ni moja ya mikakati yake ya kukuza muziki wa kizazi kipya. Alisema kuwa studio hiyo itatoa nafasi kwa wasanii tofauti tofauti wakiwemo pia wasanii chipukizi kurekodi kazi zao ikiwa ni sehemu ya kukuza vipaji vipya vinavyozaliwa kila siku.
Akizungumzia sababu ya kuiita studio hiyo jina la Mwanalizombe, Professa Jay aliweka wazi kuwa ameita
jina hilo ikiwa ni kuonesha mapenzi ya dhati kwa mkoa wake wa Ruvuma. Alisema kuwa yeye ni mtu wa Ruvuma na Mwanalizombe maana yake ni Mwana Ruvuma, hivyo hajakosea kuita jina hilo studio yake.