Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Madee ameweka wazi kuwa nyimbo yake ya 'Nani kamwaga pombe yangu' imemuingizia mtonyo zaidi ya milioni 140.
Akizungumza katika moja ya mahojiano ndani ya radio ya Clouds FM Madee aliweka wazi kuwa hiyo ndiyo nyimbo yake ya kipekee iliyomuingizia hela kwa muda mfupi hali iliyopelekea kubadili aina ya muziki kuacha muziki wa Hip Hop na kuamini kuwa staili anayoifanya sasa ndiyo ipo kwenye biashara.
Msanii huyo ameweza kukusanya mtonyo huo katika shoo mbalimbali ambapo aliweka mchanganuo wa shoo zake kuwa aliweza kupata shoo 8 za fiesta, pia aliweza kuingia mkataba na kampuni za simu ambapo aliweza kukusanya zaidi ya milioni 80 pamoja na kampuni ya Coca Cola.
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.








.jpg)