Google PlusRSS FeedEmail

WASTARA KUJA KWA NGUVU MPYA

                                                Wastara Juma
Wastara Juma ‘Stara’amesema ameingia kazini kwa nguvu katika hali ya kukabiliana na hali
halisi ya maisha kwani anahitaji kuhudumia familia yake pasipo kumtegemea mtu maana aliyekuwa akimsaidia hayupo tena, anasema kuwa awali alikuwa katika mapumziko falme za Kiarabu Dubai toka
arudi anafanya kazi kwa nguvu.“Nimekusudia kufanya kazi kwa nguvu ili kuwasaidia wanangu

Maisha ya sasa si ya kuwa tegemezi, namshukru Mungu watayarishaji wenzangu wananikumbuka katika kazi zao wananihita na kunipa nafasi ya kushiriki katika filamu zao na kunilipa vizuri, na nimejipangia kufanya hivyo na kuandaa kazi zangu kujikwamua kimaisha si unajua mimi ndio kila kitu kwa sasa,”anasema Stara.

Wastara hadi sasa tayari amerekodi filamu tano ambazo bado kutoka na kuingia sokoni , msanii huyo alisimama kufanya kazi baada ya kuuguliwa na marehemu mume wake marehemu Sajuki baada ya kifo cha mumewe aliondoka na kusafiri kwenda Uarabuni kwa ajili ya mapumziko, hali hiyo ilitokana na utendaji wa kazi wake na marehemu katika kampuni yao ya Wajey film hivyo alihitaji kupumzika kabla ya kuanza kufanya kazi akiwa pekee yake.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging