ZITTO AJIBU SALAMU ZA NEY WA MITEGO
HATIMAYE Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe amjibu msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Ney wa Mitego kuwa alichokiimba juu yake ni moja ya kazi yake ya sanaa
Zitto alimjibu msanii huyo kupitia ukurasa wake wa Twitter juu ya kile alichokiimba kwenye wimbo wake wa Salamu zao. Zitto alidai kuwa alichokiimba msanii huyo ni moja ya kazi ya sanaa hivyo maneno yake anayachukulia kama changamoto.
"Ney amefanya sanaa, nachukua maneno yake kama changamoto, ni kazi ya Sanaa ninayoithamini sana" hayo ndio maneno yaliyoandikwa na Zitto kwenye ukurasa wake huo wa Twitter.
Ney wa Mitego hivi karibuni ametoa wimbo unaokwenda kwa jina la Salaamu Zao ambapo moja ya mashairi yake yalimtaka Zitto kuachana na masuala ya Bongo Fleva kwani teyari ameshalitelekeza kundi la Kigoma All Stars.