Google PlusRSS FeedEmail

JAMBO SQUARDS NA LADY FIRE WATISHIWA KUUAWA NA MTU ANAYEJIITA KAKA KIBO WA ARUSHA

                            


Kundi la Jambo wamedai  kutishiwa Kuuwawa na mtu ambaye anajihisi kuwa yeye ndiye Wamemuimbia wimbo unaokwenda kwa jina la KAKA KIBO ambapo ngoma hiyo ilitungwa na Vijana hao na kupewa nafasi ya kuiimba Mdogo wao anayejulikana kwa jina la Lady Fire Manzi ya Ara. Nigger C amesema baada ya wimbo huo kuanza kufanya poa kwenye Vituo kadhaa vya radio Nchini hatimaye ametokea Mtu ambaye anadai kuwa wao wamemuimbia yeye na vitu vyote vilivyoimbwa vinamlenga yeye Direct na jina lake ni Kibo na huyo mtu alishawahi kujiita yeye ni manager wa Jambo kitu ambacho wao kiliwaudhi na hatimaye kumkataa na kukaa mbali naye ambapo kilichofuatia ni uhasama uliosababishwa na mtu huyo kuwashikia fedha zao million 3 akidai kuwa anawatengenezea future kibiashara huku akijitapa kuwa na mkwanja wa kutosha na mwishowe wasanii hao walipogundua ni mbabaishaji hatimaye walimbwaga na walipoulizia fedha zao jamaa aliwapa laki 8 tu kitu ambacho kiliwakera wasanii hao.

Nigger ameendelea kumiminika zaidi na kusema kuwa wamemrecord mtu huyo wakati akiongea na moja kati ya Viongozi wa Grand Master record Studio ambayo wanafanyia kazi wasanii hao na sauti hiyo wanayo ya Kaka Kibo huyo akisema kuwa amewatafutia Majambazi vijana hao na amewalipa advance kwa ajili ya kuwalima risasi vijana wa Jambo Squard ambao ni Nigger C na Ordinally a.k.a Kisu kikali a.k.a Jogoo Kichaa na pia kumkata miguu na mikono Mwanadada Lady Fire.

Jambo Squard wanasema kinachowauma zaidi ni kwamba mtu huyo anasema atasambaza fedha kwa Ma DJ na Mapresenter ili ngoma za jambo Squard zisipigwe na kwamba kuna kituo kimoja cha Radio Arusha ambacho kimeandika Tangazo kabisa ukutani ukiingia studio kwao kwamba wimbo wa jambo squard usipigwe....

Nigger C amesema hadi sasa wao wanafuatilia RB Kumkamata mtu huyo ambaye inasemekana ana Mabov ya kutosha kumwaga ila wao wanaamini kama YAHAYA aliimbwa na JD na hakumshtaki JD inamaanisha kuwa walikuwa wengi na wao wanawajua Kibo wengi.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging