Huyu naye wanasema kafanana naye mmmh,,,

Elly G kijana ambaye yeye toka enzi za uhai wa Kanumba alipenda kujifanananisha naye.
Kuna Wakati badala ya kuona aibu wao tunajikuta sisi ndiyo tunaona aibu, unamkuta msanii anahojiwa na Televisheni au Redio kuhusu yeye lakini bila ya uoga wala aibu utasikia ‘Nimefanana sana na marehemu Kanumba, na kila mtu ananisifia’ kauli kama hizi ni kauli za kinyonge, za kijinga zinazorudisha tasnia ya filamu nyuma badala ya kusonga mbele.
Wengi wanajiuliza hao ambao wamefanya mtaji kwa kujifananisha na marehemu Kanumba wanafaidika na nini kwa kujifananisha naye au ni njia ya biashara kwao ambayo siku yoyote inaweza kufa na kupotea kabisa, au bila kutaka jina la msanii nyota hawana jipya wala maarifa ya kutoka?
Hauwezi kuvaa viatu vya mtu bila kumjua vema, wengi ambao wanajaribu kujifananisha na Legend Kanumba walimjua tu kwa sababu alikuwa ni msanii mkubwa na nyota lakini hakuna hata mmoja aliyemsoma na kumfahamu kama ni mtu wa watu na aliweza kuishi na wanahabari pamoja na wapenzi wa filamu kwa ukaribu ikiwa kujitokeza kwao katika mambo yao.

Hizi ni sehemu ya kazi zao ambazo zinawafanya watamani kuwa kama Kanumba

STORY NA PICHA KWA HISANI YA FC