MSANII kutoka nchini Marekani ambaye haishi na vituko Lady Gaga hivi karibuni ameuzungumzia ugomvi wake na msanii mwenzake Madonna na kudai kuwa hajali kuchukiwa na muimbaji huyo.
Lady Gaga amedai hayo hivi karibuni baada ya mashabiki wengi kutaka kujua chanzo cha ugomvi huo na analichukuliaje suala la yeye kutokuelewana na muimbaji huyo.
Akijibu swali la mtangazaji wa SiriusXM, Howard Stern, juu ya chanzo cha ugomvi huo, na kuulizwa kama ni wivu ndio unaopelekea Madonna kumchukia, Gaga alidai kuwa muimbaji huyo anakasirika zaidi juu yake kutokana na yeye kutoonesha hali ya kuchukia.
"Sioneshi hali ya kuchukia pindi yeye anapoonesha chuki kwangu, sioni sababu nyingine ya ugomvi na ukweli ni kwamba Madonna ni kweli ananichukia huwa anipendi kwa sababu sijali kwamba hapendi hilo inazidi kumpa chuki" alidai Gaga.
Katika moja ya mahojiano ambayo alishawahi kufanya Madonna mwaka jana muimbaji huyo alidai kuwa Gaga alikataa mwaliko wake wa kuimba pamoja, hiyo huenda ikawa ni sababu ya ugomvi wao.