Google PlusRSS FeedEmail

JUSTIN BIEBER KUTOA WIMBO NA R. KELLY



BAADA ya kukaa kimya kwa muda mrefu mfalme wa R&B  kutoka nchini Marekani Robert  Kelly hivi karibuni anatarajia kutoa wimbo kwa kushirikiana na muimbaji mdogo wa kiume ambaye haishi vituko Justin Bieber.

Muimbaji huyo alithibitisha juu ya kufanya kazi hiyo moja kwa kushirikiana na msanii huyo mdogo ambaye anamafinikio katika kazi ya muziki baada ya kuenea kwa uvumi wa kutoa nyimbo moja hivi karibuni.

Katika mahojiano yaliyofanywa na VIBE mwanzoni mwa wiki hii katika sherehe ya kusikiliza albam yake mpya inayojulikana kwa jina la 'Black Panties' inayotarajia kutoka mwishoni mwa wiki hii.

Kelly amethibitisha kufanya kazi pamoja na muimbaji huyo baada ya kuwepo kwa uvumi juu ya wawili hao kufanya kazi ya kushirikiana ambayo wanatarajia kuachia nyimbo hiyo hivi karibuni ingawa jina la nyimbo hiyo bado halijawekwa wazi.

Kwa upande wake Justine Bieber amethibitisha hilo kuwa kuna wimbo utakuja hivi karibuni walishirikiana na muimbaji huyo ambapo alitoa uthibitisho huo kupitia ukurasa wake wa Twitter.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging