MSANII wa Hip Hop kutoka nchini Marekani Kanye West amelipa zaidi ya shilingi milioni 400 kwa ajili ya watu wanaompamba mama watoto wake Kim Kardashiana .
Msanii huyo ambaye amekuwa akisindikizwa na mchumba wake katika ziara zake mbalimbali za kimuziki nchini Marekani ambapo amekuwa akihakikisha kuna watu kwa ajili ya kumpamba nywele Kim na kumfanyia make-up kwa mitindo yote mahali popote wanapohitajika.
Chanzo kimeutonya mtandao wa RadarOnline.com kuwa Kanye anatumia kiasi chochote kuufanya muonekano wake kuwa tayari kwa upigaji picha mkubwa muda wowote akitaka hivyo .








