Google PlusRSS FeedEmail

SITOKI NA MRISHO NGASA- SNURA MUSHI

                                            Snura Mushi
Snura Mushi mama wa Majanga, amekanusha uvumi ambao umeenea kuwa ana mahusiano ya kimapenzi na na mchezaji wa mabingwa wa ligi kuu Yanga sc Mrisho Ngasa, Snura amesema kuwa alikuwa kimya bila kuongelea suala hilo lakini ameona kuna baadhi ya watu wanataka kuhalalisha jambo hilo hivyo lazima alikanusha kwa nguvu zote.

           Snura Mushi


“Wapo wengi ambao najua watu watasema kuwa wacheza mpira ni mabwana zangu lakini hakuna ninayetoka naye kimapenzi, mimi sitoki na Mrisho Ngasa lakini nimefanya naye kazi ya filamu yangu ya Majanga sasa watu wanatangaza kama Ngasa ni mtu wangu na natoka naye lakini Ngasa ni msanii tu aliyeshiriki katika filamu yangu,”anasema Snura.

                Snura Mushi na Mrisho ngasa
Snura anadai kuwa katika filamu yake ya Majanga Mrisho Ngasa kaigiza kama mmewe au mchamba wake, hivyo iwe kwa bahati mbaya au kuna mtu ambaye aliwaona katika baadhi ya picha na kutangaza kuwa ni wapenzi amekosea msanii huyo anasisitiza kuwa Mrisho amemwigiza katika fani ya uigizaji ni rafiki wa kikazi tu na si vinginevyo.

               Mrisho ngasa.
Msanii huyo ambaye anafanya vizuri katika filamu na muziki hivi sasa nyota yake imeng’ara katika muziki na anatamba na kibao ‘Nimevurugwa’ huku kibao cha Majanga kukiendeleza kwa kukitungia filamu iliyoshirikisha watu maarufu kama akina Mrisho Ngasa ambaye inasemekana anatoka naye naye anasema ni filamu tu...

KWA HISANI YA FC..

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging