Google PlusRSS FeedEmail

KUMBE PAPA FRANCIS ALIWAHI KUWA BAUNSA ARGENTINA!




KATIKA hali ambayo si ya kawaida Mkuu wa kanisa Katoliki Dunia, Papa Francis inasemekana kuwa aliwahi kuwa mlinzi 'baunsa' katika kumbi za starehe nchini Argentina.

Alikili kufanya kazi hiyo wakati alipokuwa akihotubia wakatoliki waliokuwa wamekusanyika nje ya jiji la Rome, Italy mapema mwisho wa wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa CNN. papa aliwahi pia kufanya kazi za usafi ikiwa ni pamoja na kufagia lakini pia kufanya majaribio ya kemikali katika mahabara, hayo yote aliyazungumza Papa Francis katika ushuhuda wake wa 'papa wa watu' lakini pia kama kiongozi wa jumuoya ya Jeswiti huko Argentuna.

Kwa mujibu wa mwandishi wa vitabu, Christopher Lowney, alidai kuwa Papa alikuwa akiamka saa 11;30 asubuhi kila siku kwa ajili ya kufua nguo za wahuiri wake.

Pamoja na hayo Papa hakutoa maelezo ya kina kuhusu kazi yake kama baunsa na kwamba vinahusianaje na kazi yake ya leo kama Papa Mtakatifu na mtumishi wa Kristu lakini pia mkuu wa Kanisa Katoliki duniani.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging