Google PlusRSS FeedEmail

MIKE TYSON AZUIWA KUINGIA UINGEREZA



BINGWA wa zamani wa ngumi za uzito wa juu Mike Tyson amejikuta katika wakati mgumu baada ya kuzuiwa kuingia nchini Uingereza kwa sababu amewahi kupatwa na hatia ya kutumikia kifungo miaka mitatu.

Kutokana na hali hiyo ya kuzuiliwa kuingia nchini humo, Tyson amejikuta akilazimika kujiondoa katika tukio la kujinadi nchini humo, baada ya makosa ambayo anadaiwa aliwahi kuyafanya akiwa humo.

Tyson alitarajiwa kuhudhuria tukio la kutangaza kitabu chake ambapo kutokana na hali hiyo bingwa huyo wa zamani ameladhimika kusimamisha zoezi hilo nchini humo.

Inadaiwa kuwa bondi huyo wa zamani alishawahi kutumikia kifungo jela miaka mitatu baada ya kuhukumiwa kwenda jela miaka 6 kwa kosa la kumbaka msichana kwenye jimbo la Indiana nchini Marekani mwaka 1992. Amejikuta akizuiwa kuingia nchini humo kutokana na sheria za uhamiaji wa nchi hiyo ambapo inadaiwa kuwa mtu yoyote ambaye amehukumiwa kifungo cha zaidi ya miaka minne haruhusiwi kuingia nchini humo.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging