Google PlusRSS FeedEmail

BEYONCE KUABUDU DINI YA MASHETANI


MWANAMUZIKI kutoka nchini Marekani Beyonce Knowles, ambaye ni mke wa msanii wa Hip Hop nchini humo Jay Z amekiri kuwa ni miongoni mwa watu wanaoabudu dini inayoabudu mashetani inayojulikana kwa jina la 'Illuminati'.

Ameweka wazi juu ya kuabudu dini hiyo hivi karibuni katika kipindi cha mahojiano kilichofanywa na mtangazaji maarufu nchini humo Oprah, ambapo alidai kuwa ni miongoni wa waumini katika kundi linaloitwa 'New World Order' ambao wanajulikana kwa jina la Illuminati.

Oprah alimuuliza swali hilo muimbaji huyo baada ya kuwepo na uvumi juu ya muimbaji huyo kuwepo na uhusiano na kundi hilo linaloabudu mashetani, na kudai kuwa kuna sababu zinazopelekea yeye kufanya hivyo.

Kwa hali ambayo si ya kawaida baada ya kuulizwa swali hilo muimbaji huyo Beyonce alianza kufanya mambo yanayofanywa na kundi hilo la Illuminati.

Kwa mujibu wa mtandao wa Huffington, umedai kuwa umaarufu pamoja na mafanikio ya muimbaji huyo umesababishwa na msaada wa dini hiyo inayoabudu mashetani.

Inasemekana kuwa muimbaji huyo aliamua kufunguka na kuweka wazi shukurani zake kutokana na mafanikio yake pamoja na kuwashukuru wote waliokuwepo nyuma yake kwa msaada wao.

"Watu wanajiuliza siri ya uzuri na muonekano wangu usiozeeka ni kwa sababu ya hizi damu ninazokunywa katika sadaka na matoleo" alisema Beyonce.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging