MWANAMUZIKI kutoka nchini Uganda Juliana Kanyomozi yupo katika maandalizi ya mwisho ya kuandaa nyimbo zake mpya kwa ajili ya mashabiki wake kwa mwaka huu wa 2014.
Muimbaji huyo ambaye ni miongoni mwa majaji wa mashindano ya kuimba ya Tusker Project Fame amewapa taarifa mashabiki wake kuwa wajiandae kupokea kazi zake hizo anazoamini zitafanya vizuri katika soko la muziki ndani na nje ya Uganda.
Juliana ambaye kwa kipindi cha mwaka jana alikuwa katika misukosuko ya kimapenzi hali iliyopelekea kushindwa kufanya vyema kwenye kazi zake za muziki kama ilivyozoeleka.
Mwanamuziki huyo mwaka jana aliweza kushiriki vyema katika mashindano ya Tusker kama jaji , ingawa alikumbwa na misukosuko ya kimapenzi hali iliyopelekea kuachana na baba wa mtoto wake mmoja hali hiyo ilimuumiza hadi kupelekea kuandika wimbo kuhusu hatua hiyo.
Juliana alituma picha kwenye ukurasa wake wa facebook, ikimuonesha yupo studio akirekodi nyimbo.








