Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Ommy Dimpoz amepata mualiko wa kufanya shoo jijini London Uingereza siku ya 'Valentine's Day' ambapo show hiyo imepewa jina la 'Valentines Zone.
Shoo hiyo inatarajia kufanyika siku ya 15 Februali huku akiwa amesindikizwa na mtangazaji mwenye machachali nchini Salama Jabiri ambaye ndiye atakayeongoza shoo hiyo.
Msanii huyo ambaye anatamba na nyimbo zake ikiwemo Tupogo, Me and You, amedai kuwa watakao hudhuria shoo hiyo watapata burudani ya aina yake kutokana na maandalizi mapya anayoyafanya kwa ajili ya shoo hiyo.








