BAADA ya ukimya wa muda mrefu hatimaye msanii wa muziki nchini Kenya David Mathenge 'Nameless' anatarajia kutoa albamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Before I Retire' hivi karibuni.
Kwa mujibu wa mtandao unaoandika story za burudani 'Niaje' wa nchini Kenya ulidai kuwa msanii huyo yupo mbioni kuachia albamu hiyo itakayobeba nyimbo 20 tofauti tofauti.
Ikiwa bado wasanii wa 'bongo' wanalalamikia kuingia hasra kwa mauzo ya albamu msanii huyo kutoka nchini huko Kenya amedai kuwa albamu hiyo ambayo itaonesha upande wa pili wa maisha yake.
Msanii huyo ambaye amewahi kufanya vizuri kwenye sekta ya muziki ndani ya nchi kwa kutamba na nyimbo zake ikiwemo Sinzia, pamoja na Salary yupo katika hatua za mwisho za kuikamilisha albamu hiyo.








