NEY WA MITEGO 'MATATANI'
Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini miondoko ya Hip Hop, Ney wa Mitego amejikuta akiingia matatani kumpoteza mpenzi wake Siwema 'Wemalious' mara baada ya kutoa video yake mpya ya 'Nakula ujana'.
Hali hiyo imeibuka hivi karibuni mara baada ya msanii huyo kuachia video hiyo ambapo moja ya picha inamuonesha msanii huyo amezungukwa na wasichana watano kutoka Kenya wakiwa wamemshika kifuani, huku msanii huyo akiwa hajavaa nguo kifuani kwake.
Kutokana na jambo hilo mwanadada huyo alionesha hali ya kuingia na wasiwasi kupoteza penzi hilo ambalo linaonekana kuota mizizi baada ya msanii huyo kuonekana kujiachia na warembo hao.
Hali hiyo ilimsababisha msanii huyo kuandika katika ukurasa wake wa Instagram ili kumtoa wasiwasi mpenzi wake "Nakula ujana video inataka kuharibu kwa bby, sikiliza Mrs Nay hii ni video tu, hakuna kingine kilichoendelea baada ya hapo ni kweli wewe ndio unayestahili kushika hicho kifua ila ni kazi tu na nilitaka kufanya kitu kizuri, naomba tusigombane kwa sababu ya hiyo video, sawa angeweza kuigiza mtu mwingine ila sijaona haja ya kumuweka mtu nilitaka kuonesha uhalisia kidogo,@wemalious mimi nakupenda wewe sana kila mtu anajua, wale mabinti wa kikenya wasikupe wasiwasi" aliandika Ney wa Mitego








