MSANII wa kike wa muziki wa kizazi kipya nchini ambaye pia alishawahi kuwa mtangazaji Rehema Chalamila 'Ray C', amejikuta katika wakati mgumu mara baada ya kushindwa kuchagua aendelee na fani ipi.
Ray C amekiri kutamani kurejea tena kwenye fani yake ya utangazaji, ambayo ndiyo miongoni mwa kazi aliyoanza nayo kabla ya kujitika katika masuala ya muziki yaliyompa umaarufu nchini na ndani ya nje.
Msanii huyo amejikuta akishindwa kufanya maamuzi hali ambayo imempelekea kuomba ushauri kwa mashabiki zake kama angeweza kuendelea na fani ya utangazaji au kufanya zote kwa wakati mmoja.
"Utangazaji nilianza 1999 muda mrefu najivunia nilipitia mengi hadi leo hii nikikaa nikifikiria kazi nilizopitia huwa najisikia raha sana, kwa sasa muziki upo kwenye damu yangu ingawa naweza kufanya vyote na wakati huo huo nikawa na kipidi changu nani ya radio, tv mnafikiriaje nifanye vyote kwa pamoja au" swali hilo ameuliza muimbaji huyo kupitia ukurasa wake wa instagram.
Kupitia swali hilo mashabiki mbalimbali walijitkeza kumuunga mkono msanii huyo na baadhi yao kumtaka kurejea kwenye pande zote mbili na kuonesha uwezo wake wa kuimba na kutangaza.








