Google PlusRSS FeedEmail

HUYU NDIYE MWANAUME ALIYEMPA LIL KIM MIMBA


BAADA ya rapa wa kike Lil Kim kuonesha kitumbo chake kuwa ni mjamzito, huku kukuzia maswali mbalimbali na tetesi za kutaka kujua  baba halisi wa  huyo mtoto mtarajiwa

Maswali hayo yalipata majibu ambapo mwanamuziki kutoka Marekani anayejulikana kwa jina la Paper amefunguka kwenye mahojiano yaliyofanyika "The rickey smiley Morning Show" kuwa yeye ndiye baba wa mtoto huyo mtarajiwa.

“Tuko pamoja. Kila kitu kiko poa. Huyo ni mke wangu na huyo ni mtoto wangu.” Alisema Mr. Papers na kuongeza kuwa Lil Kim ana ujauzito wa miezi takribani sita na kwamba wanatarajia kupata mtoto kati ya mwezi May au June.

Rapper huyo aliiweka wazi jinsia ya mtoto huyo kwa kutumia kiwakilishi cha jina kinachomaanisha kuwa ni mtoto wa kiume na kumsifia kuwa atakuwa ‘Gemini’, yaani mtoto aliyezaliwa katikati ya mwezi May na June lakini mbunifu na mwenye akili.

Hata hivyo hakutaka kutaja jina la mtoto walilolichagua, “ila tutawafahamisha wote hivi punde.”

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging