Google PlusRSS FeedEmail

KALA JEREMIAH AMRUDIA MUNGU



MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Kala Jeremiah afanya maombi ya kumshukuru mungu mara baada ya kunusurika kwenye ajali mbaya ya gari iliyotokea usiku wa siku ya Wapendanao, Februali 14.

Msanii huyo wa miondoko ya Hip Hop alinusurika kwenye ajali hiyo baada ya gari lake alilokuwa akiendesha kuingia mtaroni baada ya kufanya jitihada za kumkwepa muendesha pikipiki  ambapo ilipelekeea mlango wa upande wa kulia kuvunjika.

Akizungumza na Pro -24,  msanii huyo alisema kuwa ameamua kufanya ibada ya kumshukuru mungu kwa kumnusuru kwenye ajali hiyo, ambapo ametoka akiwa hana jeraha lolote mbali na maumivu kidogo kichwani.

Alisema kuwa ajali hiyo ilitokea mida ya saa nane na nusu usiku, maeneo ya Banana Ukonga jijini Dar es Salaam akitokea kwenye tamasha la Valentine lililofanyika Club East 24 Mikocheni, Dar es Salaam.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging