Google PlusRSS FeedEmail

UGOMVI WA TYRESE NA MKE WAKE WA ZAMANI POLISI WAINGILIA KATI


Muimbaji wa miondoko ya R&B ambaye pia ni muigizaji wa Fast and Furious Tyrese Gibson ameingia kwenye mtafaruku tena na mke wake wa zamani Norma Gibson hali iliyopelekea polisi kuitwa ili kusuruhisha mzozo huo.

Kwa mujibu wa TMZ, Norma ndiye aliyewaita polisi baada ya Tyrese kufika nyumbani kwake akitaka kumchukua binti yao Shayla mwenye umri wa miaka 6 kwa mujibu wa ratiba ya kumtembelea, lakini Norma alimzuia kwa kuwa mtoto huyo alikuwa mgonjwa.

Majibishano yaliongezeka na polisi walipofika mambo yalienda vizuri ambapo chanzo kimoja kimeiambia TMZ kuwa amani ilikuwepo na hakuna maelezo yaliyochukuliwa na polisi kwa ajili ya mashitaka.

Hata hivyo, chanzo cha kilichoaminiwa na TMZ kimedai kuwa Tyrese anaamini kuwa mtoto huyo hakuwa anaumwa bali mama yake alitaka asimchukue, na kwamba amewahi kufikiria kumfungulia mashitaka na kumfunga Norma kwa madai kuwa amekiuka amri ya malezi.

Tyrese na Norma walikuwa wapenzi tangu mwaka 2003, na walimpata mtoto wao Shayla mwaka 2007. Lakini wawili hao walilazimika kutengana mwaka 2009.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging