MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini anayejulikana kwa jina la Roma anayetamba na wimbo unaojulikana kwa jina la KKK amefunguka na kueleezea wimbo huo ambao umejaa mashairi yenye utata.
Moja kati ya mistari hiyo ni mistari inayomtaja Lady Jay Dee kwa jina la ‘Jide’ na rapper wa Tamaduni music ‘Songa’, mistari ambayo ilikosolewa na P The MC wiki iliyopita kwa madai kuwa haiwezekani Roma ashangae Jide kumjua Songa wakati yeye pia ameanza muziki miaka aliyoanza Songa na bado Jide anamjua (Roma) na hakuna anayeshangaa.
Kwa mujibu wa kipindi cha Bongo Dot Home 100.5 times Fm, Roma alifafanua kuwa ameweka mstari huo kwenye nyimbo yake hiyo ikiwa ni mahususi ya kutoa matabaka kwa wasanii waliotangulia.
“Hiyo mistari miwili, ‘wanatugawa kimakundi watumeze ona Anaconda...leo Jide anamjua Songa’. Game yetu inakuwa inashikiliwa na wadau, wadau wanakuwa wana-run game yetu, inakuwa kama formula.” Amesema Roma.
“Verse ya pili nimeongea kuhusu umoja wa wasanii, ili uweze kuwatawala watu wale watu wakiwa kwa pamoja, wakiwa na nguvu moja wana kauli moja na lugha moja kuwatawala ni ngumu sana. Ila wakiwa vipande vipande ni rahisi sana. Sasa game yetu imetengenezewa mazingira hayo ikawa ina matabaka. Halafu mifano mingi sana ipo ambayo tumeweza kuishuhudia kwamba kuna matabaka kati ya wasanii hawa na hawa.” Ameongeza.
Ameeleza kuwa kunapokuwa na matabaka kati ya wasanii inakuwa rahisi kutawaliwa na kwamba kuna watu ambao wanawagawa wasanii katika makundi mbalimbali ili iwe rahisi kuwatawala.
Rapper huyu akaweka msisitizo kwenye maana ya kuonesha mshangao baada ya Jide kumjua Songa wa Tamaduni Music. Roma ameeleza kuwa pasingekuwa na tatizo kati ya wasanii na kungekuwa na umoja wasanii basi kungekuwa na umoja na ingekuwa vigumu kufahamiana mmoja mmoja.








