Google PlusRSS FeedEmail

SHILOLE KUJA NA MGAHAWA WA CHUNA BUZI


MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Shilole anatarajia kufungua mgahawa atakao upa jina la 'chuna buzi cafe' , ili kuondelea kujitafutia kipato kwa ajili ya kujiendeleza kimaisha.

Msanii huyo ambapo anatarajia kuufungua mgahawa huo ikiwa ni siku chache tu kuuachia wimbo wake mpya unaojulikana kwa jina la Chuna Buzi.

Shilole alifunguka na kudai kuwa anatarajia kufungua mgahawa huo wa chakula maeneo ya nyumbani kwao Mwananyamala jijini Dar es Salaam, ingawa ikumbukwe kuwa si kwa mara ya kwanza kufungua vitu mbalimbali vya biashara.

Msanii huyo hapo awali alishawahi kufungua bar maeneo ya Mwananyamala ambapo haikuweza kukaa muda mrefu, na aliifunga bila ya kuweka wazi ni sababu gani zilipelekea kufungwa kwa baa hiyo ambayo ilijizoelea umaarufu.

Aliweka wazi kuwa mbali na kuwa mwanamuziki pia anataaluma ya kuendesha masuala ya hoteli, kwani alishawahi kuwa mama ntilie kipindi kilichopita ikiwa ni moja ya njia ya kujitafutia kipato.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging