Google PlusRSS FeedEmail

DRAKE AMNUNULIA RIHANNA PETE YENYE THAMANI 68 MILIONI

            
Drake na Rihanna penzi lao linachanua huku wakiripotiwa kuwa na mpango wa kuishi pamoja.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Star, chanzo kimoja kimeeleza kuwa Drake amemnunulia Rihanna zawadi ya pete ya almasi yenye rangi ya njano yenye thamani ya $42,000 (sawa na 68,712,000/-).


Hata hivyo imeelezwa kuwa pete hiyo sio ya uchumba.
“Rihanna aliikubali zawadi hiyo kama ishara ya mapenzi ya Drake. Sasa hivi (Drake) anabadili hata ratiba zake ili atumie muda mwingi ipasavyo kuwa na Rihanna.” Kilieleza chanzo hicho.


Drake na Rihanna wanaonekana kuwa karibu zaidi kadiri siku zinavyozidi kwenda, na hata Jumapili katika MTV Movie Awards walionekana wakiwa wameshikana mikono muda mfupi baada ya Drake kuperform.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging