![](http://www.jhikoman.com/img/ZIFF2013-Jhikoman.jpg)
Baadhi ya festival zitakazo funikwa na mwanamuziki huyo ni Helsink Film Festival kule Finland, na Norway na imebainika kuwa Jhikoman pia atashirikiana jukwaa na wazee wa kazi FFU Ughaibuni a.k.a "watoto wa mbwa" Ngoma Africa band katika maonyesho makubwa ya Tubingen,Ujerumani yatakayo fanyika kuanzia 17 mpaka 20 Julai 2014.
Hivi karibuni, Jhikoman na bendi yake ya Afrikabisa Band, ametajwa kuwa ni balozi nyota bora ya Reggae anayekubalika kimataifa na anaweza kumudu kutingisha jukwaa lolote kubwa la kimataifa.