Google PlusRSS FeedEmail

JINA LA LULU LATUMIKA KUTAPELI WATU



MSANII wa filamu nchini  Elizabeth ‘Lulu’ Michael ameelendelea kuwa mmoja kati ya waathirika wa vitendo vinavyofanywa na watu wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii kwa majina ya watu maarufu kwa lengo la kujipatia fedha.

Watu hao ambao wanafungua akaunti mbalimbali kwenye Facebook kwa jina la Elizabeth Michael wamepost maelezo yanayoonesha kuwa muigizaji huyo ameendelea kuchangisha fedha kwa ajili ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu na kutaja kiwango ambacho wameshakipata huku wakiomba watu waendelee na moyo huo.

Lulu amepost kwenye Instagram ujumbe uliowekwa na matapeli hao kwenye ukurasa wenye jina lake.

“Nawashukuru wale wote mlioungana na mimi siku ya juzi (Jumatatu. Pia ninawashukuru wote mliochangia mfuko maalum nilioanzisha ili kusaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi. Jumla ya pesa iliyopatikana ni 3.7m /= hadi kufikia jana (Juzi). Lakini kwa wale wanaohitaji kuendelea kutuma mchango wao ili kusaidia hawa watoto wetu wanaweza kutuma mchango wao kwa tigopesa namba 0714152844.” Inasomeka sehemu ya ujumbe huo.

Muigizaji huyo ameandika kwenye Instagram kuwatahadhalisha watu dhidi ya matapeli hao ambao anadai wamepost video ya ngono kwenye ukurasa huo ikionesha kuwa yeye ndiye kafanya hivyo.

“Morning ma pipo....dah sijui niseme vp...hizi facebook accounts sio zangu...kama huyu anaomba michango eti...dah the same account ipe post video ya ex.....na ziko account nyingi sana....nwei ni hv mm sina account yoyote facebook nina fan page moja tu ELIZABETH LULU MICHAEL....kwahyo kuweni makini na hao matapeli...na nyie mnaotumia jina langu vibaya I thnk ts time to lv me alone...kwa hayo mapenzi ya kutumia jina langu ovyo nimeshindwa mm....!!” Lulu ameandika.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging