“Tuache kulalamika wakati tunavunja sheria zilizowekwa na zipo katika Katiba yetu ya Tanzania, haiwezekani kila mtu akafanya anavyotaka mwenyewe wakati kuna vitu vinaenda tofauti, kila jambo lina utaratibu wake wa kufuatwa ili mila, Desturi zilindwe, hivyo tuiache Bodi ifanye kazi yake,”anasema Mzee Chilo.
![](http://2.bp.blogspot.com/-Wz_ldfmBma8/UcRsGMu_mbI/AAAAAAAAhiI/U1J5kLINQKo/s640/Bi.-Joyce-Fissoo.jpg)
Mzee Chilo alisema hayo wakati akichangia katika mjadala uliandaliwa na Serikali wakitathimini hali ya soko kwa sasa Tanzania, amesema kuwa wasanii na watayarishaji wawe makini kwa kusoma kanuni na sheria yenyewe ya filamu inasemaje kabla ya kwenda location na kutengeneza sinema ambayo ikija kukaguliwa inakosa sifa za kuingia sokoni na badala yake watu wanaanza kulaumu bodi wakati hawakufuata taratibu.