![](http://www.bongocelebrity.com/wp-content/uploads/2011/08/GURUMO-MUHIDIN.jpg?width=450)
Taarifa zilizothibitishwa na hospitali ya Taifa Muhimbili zimesema Mzee huyu amefariki Dunia akiwa hospitalini hapo saa nane mchana baada ya kufikishwa Hospitalini hapo April 12 asubuhi na kulazwa kwenye wodi namba 6 ya Mwaisela kutokana na kuzidiwa.
Tayari mwili wake umepelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti ambapo mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumatatu April 14 huko Masaki Kisarawe Katika kijiji alichozaliwa.
Pro24 inatoa pole kwa familia ya mzee Gurumo na wapenzi wa Bendi yake Msondo Ngoma,Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pepa peponi Amina