Google PlusRSS FeedEmail

MAFURIKO YAMSABABISHA JAYDEE KUSIMAMISHA UZINDUZI


MVUA inayoendelea kunyesha kanda ya Pwani hususani eneo la Dar es Salaam imeripotiwa kusababisha athari kubwa ikiwemo uharibifu wa makazi pamoja na miundo mbinu huku baadhi ya familia wakipoteza ndugu zao.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Lady Jaydee ni mmoja katika watu walioathirika na mvua hiyo hali iliyopelekea kumlazimu kuhairisha uzinduzi wa nyimbo yake mpya.

Jaydee alipanga kuzindua nyimbo yake mpya mwishoni mwa wiki iliyopita lakini kutokana na mvua kunyesha huku kukiwa kumejitokeza athari kubwa zilizosababishwa na mvua hizo, msanii huyo imemlazimu kuhairisha zoezi hilo.

Jaydee ametangaza kupitia ukurasa wake wa facebook, kuwa amesimama kuzindua kazi hizo ambapo alikuwa azindua audio, pamoja na video ya wimbo 'Nasimama'.

Msanii huyo aliwapa mashabiki wake taarifa kupitia ukurasa wake huo wa facebook juu ya kuhairisha kwa uzinduzi huo kutokana na mvua zinazonyesha jijini.

"Nasikitika kutangaza kuahirisha kwa shughuli ya utambulisho wa wimbo na video mpya ya Jaydee 'Nasimama', kutokana na ahali tete ya bojo iliojitokeza ambayo iko nje ya uwezo wa kibinadamu, lakini wimbo na video vitarushwa leo katika mtandao." aliandika Jaydee.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging