Baada ya wimbo wa 'Happy' ulioimbwa na Producer Pharrell Williams kuonekana ni miongoni mwa nyimbo zilizofanikiwa kwa kuwa na wamashabiki wengi, mumbaji wa nyimbo hiyo adondosha machozi.
Mafanikio hayo ya wimbo huo yalimpelekea muimbaji huyo kutoa machozi ya furaha wakati akifanya mahojiano maalumu na mtangazaji mkongwe wa Oprah Winfrey katika kipindi chake cha Oprah Prime'.
Baada ya Oprah kumuonesha video ya jinsi mashabiki wake wa sehemu mbalimbali dunia walivyoupokea wimbo huo kiasi cha kusababisha wimbo huo kuwa mkubwa hali iliyopelekea kupata mafanikio makubwa.
Kitendo hicho ndicho kilichopelekea msanii huyo kutoa machozi ya furaha huku akiwa aamini kitendo hicho ambacho ni moja ya mafanikio makubwa katika kazi yake ya muziki.
Akiwa anafuta machozi alisema kuwa "nashukuru kufahamu kwamba watu wameniamini kwa kipindi kirefu sana, mpaka kuweka kufikia hatu hii mpaka kujisikia hivyo".