Google PlusRSS FeedEmail

PROFESSOR JAY AJIANDA KUTOA ALBAMU MPYA


MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini miondoko ya Hip Hop, Joseph Haule 'Professor Jay' yupo katika hatua ya mwisho ya kutoa albamu yake mpya ambayo itakamilisha albamu ya tano tangu aanze kazi ya muziki.

Ikiwa bado tatizo la usambazaji wa albamu za muziki nchini ikionekana ni tatizo kubwa kwa baadhi ya wasanii huku baadhi yao wakilalamika kupata hasara Professor Jay ameweka wazi uwamuziki huo wa kutoa albamu yake mpya mwaka huu.

Akizungumza na jarida hili Professor Jay aliweka wazi kuwa yupo katika maandalizi ya mwisho kutoa albamu yake mpya itakayotimiza idadi ya albamu ya 5 huku akiweka wazi kuwa atafanya kazi hiyo ya kuisambaza mwenyewe.

Msanii huyo hivi karibuni ametoa wimbo alioupa jina la 'Kipi sijasikia' akiwa amemshirikisha Diamond, huku akiweka wazi kuwa atatumia mbinu zilizotumiwa na baadhi ya wasanii akiwemo Jaydee katika kuhakikisha albamu yake inawafikia mashabiki pamoja na kupata faida.

"Hivi sasa nimejipanga kwa ajili ya kutoa albamu yangu nyingine ingawa kuna ugumu wa kutoa albamu kwa kipindi hiki ila nitajipanga kwa ajili ya kuhakikisha albamu inawafikia mashabiki wangu na mimi pia kupata faida" alisema Jay.

"Nitatumia njia aliyoituma dada mkuu Jaydee, kama Mrisho Mpoto aliweza kuuza albamu na naamini kuwa na mimi nitaweza kuuza kwa kutumia njia hiyo " alisema Jay.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging