Google PlusRSS FeedEmail

RICH MAVOKO KUFANYA SHOW NJE YA NCHI



MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Rich Mavoko yupo katika maandalizi ya mwisho ya kujipanga kufanya show za muziki barani ulaya ambapo show hizo hazitapungua 8.

Hali hiyo inaonesha kuwa muziki huo wa kizazi kipya nchini unalipa kwani hivi sasa orodha ya wasnii wa muziki huo kwenda kufanya shoo nje ya nchi inazidi kuongezeka siku hadi siku huku baadhi yao kutumia fursa hiyo kwa kufanya collabo na wasanii mbalimbali wa nje.

Mwimbaji huyo anayetamba na kibao cha  Roho Yangu, Rich Mavoko ana kila sababu ya kufurahia matunda yanayoendelea kuongezeka katika shina la muziki mzuri anaoufanya ambapo hivi sasa  ataingia barani Ulaya kufanya shows zisizopungua nane ikiwa ni kwa mara ya kwanza anafanya show nje ya bara hili.

Kwa mujibu wa mtandao wa TimesFM, uliandika hivi “Mungu akijalia naweza nikaenda Europe na naenda kufanya shows kama nane hivi. Kwa hiyo my manager ndio alikuwa anahangaikia hivyo vitu…vitu vyote hivyo yeye ndiye anafanya. Kwa hiyo Mungu awabariki, nijaribu kutoka.”, hayo ni maneno yaliyozungumzwa na Rich Mavoko.

Akizungumza na Pro-24 Mavoko aliweka wazi kuwa ameipokea taarifa hiyo ikiwa ni sehemu ya mafanikio yake ambapo ameeleza kuwa hiyo ziara ni matunda ya wimbo wake wa Roho yangu ambao ndio uliompa show nyingi.

Hata hivyo, mwimbaji huyo amesema bado ni mapema kutaja nchi na tarehe rasmi atakayoondoka lakini ameshacomfirm na anasubiri kukamilisha taratibu nyingine.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging