Google PlusRSS FeedEmail

SWEBE ASHANGAZWA NA WATU WANAOTUMIA JINA LA KANUMBA KAMA MTAJI



Msanii wa filamu aliyetamba na kundi la Kaole Sanaa Group, Swebe Santana amekuwa miongoni mwa wasanii wa filamu walioandika ujumbe maalum kwa marehemu Kanumba ikiwa ni moja ya maadhimisho ya kutimiza miaka miwili tangu afariki dunia.

Swebbe ameandika ujumbe huo kwenye ukurasa wake wa Facebook kwa herufi kubwa akionesha hisia zake na mtazamo wake kuhusu tasnia ya filamu na kinachoendelea. 

Ambapo katika ujumbe huo Swebe ameonesha hisia zake kwa baadhi ya watu wanaotumia jina la Kanumba kwa ajili ya kujitafutia pesa na kuifanya siku hiyo iwe ni siku yao ya kujiongezea kipato.

"Umekuwa mtaji kwa walio hai, baada ya kuombewa dua watu wanasherehekea kwa mabendi kuyaalika huku viingilio vikitawala" aliandika Swebbe katika ukurasa wake huo

Mbali na hayo pia aliongezea kuwa “Kwa sasa filamu zinauzwa kwa majina na sura na si uwezo…yote kwa yote soko la filamu limekufa Bongo..” Inasomeka sehemu ya ujumbe mrefu wa Swebbe.

Swebbe amedai kuwa ana mengi ya kumwambia Kanumba lakini anaomba Mungu amsamehe huku akiwarushia dongo wale aliodai wanafanya dhihaka kwa kutumia jina lake.

“Zangu dua zitakufikia na Mungu mwenye sifa ya kusamehe akusamehe..na wanaofanya dhihaka juu ya hilo nao awasamehe. Hakika kwa Mungu wote tutarejea…nina mengi..lakini kwa haya machache wacha tuu nijifute chozi na dua kukuombea…R.I.P rafiki yangu mpendwa Steven Charles Kanumba.”

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging