BAADA ya ukimya wa muda mrefu zaidi ya miaka 8, kundi la wagosi wa Kaya lenye makazi yake mkoani Tanga, warejea tena katika game ya muziki wa kizazi kipya huku wakiwa teyari wamemaliza maandalizi ya albamu yao waliyoipa jina la 'Uamsho'.
Kundi hilo linaliundwa na wasanii wawili Mkoloni pamoja na Dr.John teyari wameshaachia nyimbo zao mbili zilizoambatana na video ambapo nyimbo hizo ni 'Bao' pamoja na 'Gahawa'.