Mwigizaji Nyota katika tasnia ya filamu Wastara Juma amesema kuwa wanashukuru Mungu kwa safari yao ya kikazi nchini Uingereza na wamefika salama na wapo katika jiji la London wakivinjari kwa ajili ya kujua mitaa na sehemu wanazotarajia kurekodi filamu hiyo.
Tunashukru Mwenyezi Mungu tumefika salama na tumepokelewa vizuri, tupo tayari kwa ajili ya kazi iliyotuleta kwa ajili ya kurekodi filamu mpya inayotushirikisha wasanii mahiri katika tasnia ya filamu kutoka Bongo,”anasema Stara.
Wasanii hao wapatao wane wapo nchini Uingereza kwa ajili ya kurekodi filamu inayotayarishwa na Didas Fashion & Entertainment, sinema hiyo inawashrikisha wasanii nyota kama vile Yvonne Cherryl ‘Monalisa’, Wastara Juma ‘Stara’, Riyama Ali na Issa Mussa ‘Cloud 112’ akiwa ndiye mwanaume pekee.