MSANII muigizaji wa kike wa filamu za Tanzania (Bongo Movies) anaefahamika kwa jina la Rachel Haule amefariki leo asubuhi.
Taarifa kutoka kwa chanzo chetu cha kuaminika zinaeleza kuwa muigizaji huyo alikuwa mjamzito na kwamba alijifungua kwa njia ya upasuaji (Operation) lakini kwa bahati mbaya mwanae alifariki dunia. Imeelezwa kuwa Rachel alipelekwa katika chumba maalumu cha wagonjwa mahututi ( ICU) baada ya hali yake kuwa mbaya sana na leo asubuhi alifariki pia hivyo ni msiba wa mama na mtoto.
Watu mbalimbali wameendelea kutoa pole kwa mume wa Rachel aitwae Saguda na kuonesha jinsi walivyoguswa na msiba huo.
“Sitaki kumkufur mwenyez Mungu wangu! Ila kazi yake haina makosa tulimpenda ila mwenyezi Mungu kampenda zaid! Dah inauma sana pole Saguda kwa mtihani uliokupata! Ila tupo pamoja kwa kipindi hiki kigumu.” Shilole ameandika kwenye Instagram.
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.








