Google PlusRSS FeedEmail

'KIGODORO' MARUFUKU

Hatimaye Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam limeingilia kati suala la ngoma za usiku ambazo zinajulikana kwa jina la Vigodoro.

Ambapo jeshi hilo limepiga marufuku ngoma za kitamaduni ambazo zimekuwa zikifanyika nyakati za usiku kwenye maeneo mbalimbali Dar es salaam ikiwa ni muendelezo wa kukabiliana makundi ya kihalifu ambayo yamekua tishio kwa usalama wa raia.

Kufuatia kuibuka kwa makundi ya kihalifu kama Panya road na Mbwa mwitu ambayo wengi wao wanahusishwa na ngoma hiyo kwenye uporaji na upigaji wa watu, Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Suleiman Kova anasema ‘ni marufuku kwa ngoma yeyote ya asili kuchezwa nyakati za usiku’

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging