Mvua iliyonesha siku ya Ijumaa yasababisha show iliyokuwa ikisubiliwa kwa hamu na mashabiki mbalimbali kuhairishwa, ambapo Msanii Lady Jay Dee alifikia maamuzi ya kuhairisha show hiyo kwa sababu ya mvua.
Tamasha la msanii mkongwe wa muziki nchini,Lady Jay Dee,'Historia Concert' lililofayika jana Mei 2 2014 Nyumbani Lounge limeahirishwa kutoka na mvua mkubwa iliyonyesha usiku huo.
Pamoja na hayo Lady Jay Dee aliimba nyimbo tatu kwaajili ya kuwaridhisha mashabiki waliobaki kwenye ukumbi huo huku mvua ikiendelea kunyesha na baada ya hapo aliwarudishia tiketi mashabiki hao na kuwaahidi atatangaza tarehe rasmi ya kurudiwa kwa Tamasha hilo 'Historia Concert'.
Pro-24 ilimtafuta Meneja wa msanii huyo naye alisema kuwa tarehe ya kurudia show hiyo itatangazwa tena ingawa bado hajajua lini show hiyo itafanyika