Google PlusRSS FeedEmail

NENO LA MWISHO LA TUPAC SHAKUR

Miaka takribani mingi imepita tangu Tupac Omar Shakur auwawe kwa kupigwa risasi.  Kwa mujibu wa polisi mstaafu ‘Chris Carroll, yeye ndiye alikuwa mtu wa kwanza kufika kwenye eneo la tukio na kumkuta rapper huyo akivuja damu nyingi kutokana na kupigwa risasi huko Las Vegas, Marekani.

Carroll amesimulia kupitia kitabu chake alichoandika kusema ukweli wa tukio hilo jinsi lilivyokuwa:
“Ninamuangalia Tupac, na anajaribu kumwambia kitu Suge (boss wake aliyekuwa nae wakati anapigwa risasi). Namuuliza, ‘nani kakupiga risasi? Nini kimetokea? Nani kafanya hivi?’ na alikuwa kama ananipotezea. Alikuwa ananiangalia machoni hapa na pale, lakini alikuwa anataka kumwambia kitu Suge.

“Ghafla, alibadilika. Na alianza kuhangaika akijaribu kuzungumza, na hapo ndipo nilipomuangalia na kusema tena, ‘nani amekupiga risasi?’

“Akaniangalia na akavuta pumzi kutafuta jinsi ya kusema kitu, na alifungua mdomo wake, na nilifikiri ntapata ushirikiano. Na ndipo alipotoa neno ‘F**k you’.”

Ameeleza kuwa hilo lilikuwa neno la mwisho la Tupac kwake kabla ya kuishiwa nguvu kabisa na ndipo ambulance ilipofika ikamchukua haraka na kumkimbiza hospitali ambapo ndiko alipopatwa na mauti.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging