Google PlusRSS FeedEmail

KITUKO : POLISI WAKAMATA MWANAUME AKIWA MTUPU GETI LA IKULU

Polisi wa kitengo maalum wa Marekani wamemkamata mtu mmoja akiwa ‘MTUPU’ katika geti la ikulu ya Marekani Ijumaa (May 23).

Kwa mujibu wa reporter wa mtandao wa Daily Caller ambaye anadai alikuwa anaingia pia katika geti hilo, amesimulia kuwa mtu huyo alianza kutofautiana na polisi hao wakati alipokuwa pale akiwa amevaa nguo zake na aliwaambia maafisa hao kuwa ana-appointment na Obama na kwamba anatakiwa kuonana nae saa tisa kamili mchana.

Hata hivyo kitambusho cha mwanaume huyo aliyetajwa kwa jina la Michel Bechard na maelezo yake yalikataliwa kutokana na kutokidhi vigezo.

Ndipo mtu huyo alipoendelea kusisitiza aachiwe aingie Ikulu huku akivua nguo na kudai ni lazima ahakikishe ametimiza ahadi yake na Obama kukutana muda ule.

Mtu huyo aliyetajwa kwa jina la Michel Bechard tayari ameshafunguliwa mashitaka, na imeelezwa kuwa alipelekwa hospitali kwa matibabu baada ya kupata majeraha madogo wakati akidhibitiwa na polisi hao.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging