Google PlusRSS FeedEmail

ROSE NDAUKA ANYAKUA TUZO YA MSANII BORA WA KIKE




MSANII wa filamu nchini Rose Ndauka ameibuka kidedea kwa kunyakua tuzo ya msanii bora wa kike huku akiwa amewabwaga baadhi ya wasanii wengine wa filamu akiwemo Lulu, Wema Sepetu, Wolpa, na wengine wengi.
                                   

Msanii huyo amenyakuwa tuzo hiyo ya Zanzibar International Film Festival ambapo ni miongoni mwa tamasha la filamu linalifanywa kila mwaka na kuhusisha wasanii mbalimbali kutoka duniani kote.


Akizungumza na mwandishi wa habari hii Ndauka aliweka wazi kuwa filamu iliyomfanya kushinda tuzo hiyo inajulikana kwa jina la 'Waiting Fall' ambayo ilitungwa na yeye mwenyewe pamoja na mpenzi wake.

Alisema kuwa filamu hiyo ndiyo iliyomuwezesha yeye kunyakua tuzo hiyo ikiwa bado ni miongoni mwa ndoto anazozifikiria kuwa msanii wa kimataifa na kujitangaza katika soko la filamu duniani.

Alisema kuwa anawashukuru sana mashabiki zake ambao ndio wamemuwezesha yeye kufikia hapo huku akiweka wazi kuwa bila wao asingeweza kufika katika hatua hiyo ya kuonekana kwa uwezo wake huo wa uigizaji.

Aliweka wazi kuwa tuzo hiyo ni moja ya mafanikio yake ingawa bado anachangamoto kubwa ya kuendelea kupambana katika soko hilo la filamu lililokumbwa changamoto nyingi ili aweze kufikisha malengo yake.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging