The-Dream amekumbwa na tuhuma nzito za kumpiga vibaya mpenzi wake wa zamani anaejulikana kwa jina la Lydia Nam wakati akiwa na ujauzito wa mwimbaji huyo.
Kwa mujibu wa TMZ, kitengo cha polisi cha New York kimeripotiwa kumsaka The Dream baada ya mrembo huyo kuripoti tukio hilo ambalo limeelezwa kuwa lilifanyika April 2013 katika Plaza Hotel.
Lydia amesema kuwa The Dream ambaye jina lake halisi ni Terius Nash alimpiga ngumi na mateke ili hali akiwa ni mjamzito lakini kwa bahati nzuri hakukidhuru kiumbe kilichokuwa tumboni.
Bado haijafahamika kama Lydia alifanya vipimo vya afya wakati huo na kupata vielelezo kuhusu madhara yaliyotokana na kipigo hicho. Mrembo huyo aliripoti polisi November mwaka jana.
Imeripotiwa kuwa mwezi June mwaka jana, The Dream alikamatwa na polisi kwa kosa la kumshambulia Lydia wakati wakiwa wapenzi lakini mrembo huyo hakutaka kufungua mashitaka hivyo kesi hivyo polisi waliipotezea.
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.