Google PlusRSS FeedEmail

DAVIDO ATWAA TUZO YA BEST AFRICAN ACT

UTOAJI wa tuzo za BET 2014 zimefikia tamati huku mwanamuziki kutoka Nigeria Davido kutwaa tuzo ya Best African Act.

Kipengele hicho kilikuwa kinawaniwa na mshindi huyo pamoja na wasanii wengine wakubwa Afrika ambao ni Diamond Platinumz, Mafikizolo, Toofan, Sarkodie na Tiwa Savage.

Tuzo hiyo imetolewa muda mchache kabla ya kuanza kwa show kubwa ya utoaji wa tuzo hizo inayopambwa na burudani kutoka kwa Drake, Nicki Minaj, Usher Raymond na wengine wengi.

Diamond Platinumz ambaye ameiwakilisha vizuri Tanzania licha kutopata tuzo hiyo, ameandika ujumbe wa kiushindani katika Instagram unaoonesha ukuaji katika game la kimataifa.

“Tusipopenda kukubali Matokeo na Ushindi wa Wenzetu basi Daima Hatutaweza kuwa Washindani.Muhimu ni kujua wapi tulipotoka na Wapi tulipo Leo, Katika Nchi zaidi ya 20 zenye wasanii zaidi ya Million 40, kuchaguliwa Tanzania ni fursa, Heshima na Hatua kubwa, Cha Muhimu ni kuitumia vyema Fursa Hii na Kuhakikisha Mwakani tunapiga Hatua Zaidi! Asante sana kwa wote wanaozidi kuni support kwa hali na Mali, Mapambano ndio kwaaaanza yanaanza sasa.....!!!!!! @wcb_wasafi For Life Baby.”aliandika Diamond kupitia ukurasa wake wa Instagram

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging