Google PlusRSS FeedEmail

DIAMOND TENA HIVI SASA AMEUNGANA NA MAFIKIZOLO

Diamond tena kwa mara nyingi fursa imemdondokea mara baada ya waimbaji wawili kutoka Afrika Kusini wanaounda kundi la Mafikizolo kumshirikisha Diamond kwenye nyimbo yao mpya ambayo haijafahamika kwa jina .

Fursa ya kushiriki katika tuzo za MTV MAMA mwaka huu zimezaa matunda mengine kwa Diamond Platinumz baada ya kuingia studio na kufanya wimbo na kundi la Mafikizolo ambalo lilishinda tuzo ya kundi bora na wimbo bora (Khona) .

Diamond akiongozana na meneja wake, Babu Tale waliingia katika studio za mtayarishaji maarufu wa Afrika Kusini anayefanya kazi za Mafikizolo, Oskido ambapo kazi ilifanyika.

Bado jina la wimbo na atarehe za kutoka kwa wimbo huo hazijawekwa wazi.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging