Google PlusRSS FeedEmail

EVE AFUNGA NDOA NA MFANYABIASHARA MAARUFU

RAPPER wa kike Eve hatimaye amefunga ndoa na mpenzi wake aitwae Maxmillion Cooper, June, 13 huko Ibiza, Hispania, Hii ni ndoa ya kwanza kwa rapper huyo mwenye umri wa miaka 35 lakini mumewe ana watoto wanne ambao alizaa na mkewe wa zamani.

Eve na Cooper walikuwa kwenye uhusiano kwa kipindi cha miaka 4 na walichumbiana rasmi mwaka jana, katika sikukuu ya Christmas.Cooper ambaye ni raia wa Uingereza mwenye umri wa miaka 41, ni mfanyabiashara na dereva wa mbio za magari mwenye utajiri wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 50.

Wanandoa hao walitoa tamko la pamoja kuwashukuru wageni waalikwa,“Tunafuraha iliyopitiliza kusherehekea ndoa na marafiki zetu wote na familia na kuanza safari yetu katika maisha mapya pamoja."
"Imekuwa experience nzuri sana na tunafuraha hata zaidi ya tulivyofikiria ingekuwa. "

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging