Google PlusRSS FeedEmail

KIJANA AVUA NGUO HADHARANI

WASOMI wanapokutana hasa katika zoezi la kutunukiwa cheti kama kielezo cha uhitimu wa ngazi fulani kuna vitu huwezi kuvifikiria kama vitatokea hata kidogo.

Katika Jack Britt High School, North Carolina, Marekani wanafunzi mmoja amewaacha hoi mamia ya watu waliohudhuria sherehe ya kutunukiwa vyeti (graduation) baada ya kupanda jukwaani kupokea cheti chake na ghafla akavua johon lake na kubaki na boxer.

Baada ya kuvua joho alinyoosha mikono yote miwili juu kama mwanamieleka anayetamba. Lakini haikuchukua round wanausalama wakamdhibiti na kumuweka chini ya ulinzi.

Kwa mujibu wa The Huffington Post, kijana huyo alinyang’anywa diploma yake na hivyo hakukabithiwa cheti.

Hata hivyo bado anahesabiwa kama mtu aliye maliza masomo yake na kuhitimu licha ya kuwa hana kielelezo cha elimu yake.

“Shule yetu imefanya jitihada kubwa. Hapo zamani watu waliohudhuria walikuwa wenye vurugu wakati wa graduation. Tumefanya jitihanda kuwafanya watu waheshimu wanafunzi. Huyu kijana amechagua kutoonesha heshima kwa wanafunzi wenzake.” Alisema Dr Frank Till, mwalimu wa chuo hicho

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging