Google PlusRSS FeedEmail

FLORA MVUNGI, H.BABA KUJA NA FILAMU MPYA

MSANII wa muziki wa kizazi kipya na filamu nchini, Hamis Ramadhani 'H-Baba' amesema tayari amemaliza kufanya sinema yao mpya akiwa na mkewe, Flora Mvungi ambayo imelenga kuelimisha jamii aliyoiita Umuhimu wa mama.

Akizungumza na jarida hili, nyota huyo alisema  wameipa filamu hiyo jina hilo la Umuhimu wa mama kwa kuwa maisha mama lazima awe wa kwanza katika jamii.

"Moja ya mambo mengi anayotakiwa kijana
au mtu yeyote kuheshimu ni lazima aanze
na mama, kwani mama amekuwa ndiye mkuu wa nyumba na kitovu kikubwa kwani huanza malezi katika hatua ya ujauzito wa miezi mingi mpaka kujifungua," alisema.

H-Baba alisema wasanii wengine nao wanakiwa kutengeneza filamu zenye kufunza jamii ili kutengeneza upendo wa mama nchini.

Alisema anashukuru kufunga na ndoa na mkewe Flora kwani amekuwa msaada mkubwa kwake katika kuiweka familia yake katika maelewano makubwa.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging