Google PlusRSS FeedEmail

LINEX APATWA NA WASIWASI JUU YA UTENDAJI KAZI WA SUGU BUNGENIMSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Linex Sunday 'Mjenda' ameonesha kutoridhishwa na utendaji kazi wa mbunge wa Mbeya mjini ambaye pia ni msanii wa muziki wa kizazi kipya Joseph Mbilinyi 'Sugu' tangu awe mbunge.
 
Hali hiyo inaonesha kuwa mbunge huyo wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ambaye ni mmoja wa wanamuziki wakongwe Tanzania hajamshawishi Linex Sunday Mjeda ambaye amehoji mchango wake kwenye muziki.

Linex ameandika mtazamo wake kupitia akaunti yake ya Facebook na Twitter, siku moja baada ya Sugu kumtuhumu Zitto Kabwe kwa kile alichokiita ufisadi katika TANAPA na NSSF kupitia kampuni ya Lekadutigite Ltd inayomilikiwa na wasanii wa Kigoma All Stars, akiwemo Linex.

“Hivi toka Sugu amekua mbunge ni kitu gani alishawahi kuwafanyia wasanii wa Taifa hili, Tanzania na akiwa kama waziri kivuli, amewahi kufanya nini kuinua kipato cha wasanii? Je amejenga mazingira gani kuhakikisha wasanii hawawi ombaomba wakutegemea misaada bali wajasiriamali?

"Eg. Amefikia wapi kwenye suala la hakimiliki na ufuatiliaji wake etc nimeuliza tu manaake kuna vitu vinaendelea sivielewi.”

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging