Google PlusRSS FeedEmail

HAPPINES MAGESE ATOKWA NA MACHOZI

Mrembo wa kimataifa aliyewahi kuvaa taji la Miss Tanzania, Happiness Millen Magese ametoa machozi kwa uchungu wakati akisimulia kuhusu tatizo la Endometriosis lililompelekea kuwa mgumba.

Millen Magese ameshindwa kuvumilia wakti akifanya mahojiano na Global TV ambapo ameeleza kuwa alilazimika kufanya upasuaji mara 12 na hatimaye kuondolewa kizazi.

“Nimeshafanyiwa upasuaji mara 12 na mirija yangu yote imeziba, upande wangu mmoja wa ovary haufanyi kazi. Ile ndoto yote ya mimi kama mwanamke kupata mtoto kwa njia ya kawaida imetoweka.” Amesema Happiness kwa huzuni.

Ameeleza kua aliamua kuondoa kizazi ili baadae amuasili mtoto kwa kuogopa kumuambukiza tatizo hilo mtoto ambaye angemzaa (endapo angezaa mtoto wa kike).

Amesema tukio hilo ndilo lililomsababisha aanzishe taasisi ya kusaidia wanawake wengine ili wasipate tatizo kama lake.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging